Hewala Mheshimiwa Richard Onyonka

HEWALA Mhe. Richard Onyonka(Ford Kenya) kwa kuibuka mshindi kwa kura nyingi-Kitutu Chache Kusini .Onyonka alipata kura 10,122(45.86%) .

Bwana Onyonka aliwapiku Anthony Kibagendi wa Jubilee aliyepata kura 5,074(22.99%) na Samuel Kenani(ODM) aliyepata kura 4,324 (19.59%).

 

Onyonka atahudumu muhula wa tatu mtawalia baada ya kuchaguliwa 2007 na 2013 kwa tiketi ya ODM.Kinara wa NASA Raila Odinga alimpigia debe Onyonka juma lililopita.

Seneta wa Bungoma (Kiongozi wa Ford Kenya) Moses Wetangula amempongeza  Onyonka huku akisema atamfaa bungeni.

Eneo la Kisii linaonekana kuwa ngome ya NASA kutokana na ushindi huu unaoonesha mapenzi na usemi wa watu.

Onyonka alimrithi marehemu babake Zachary Onyonka aliyeoongoza Kitutu Chache kabla ya kuwa Kitutu Chache Kusini na Kitutu Kaskazini tangu(1962-1996).

Idadi ya waliojitokeza(37.40%) ilikuwa ya chini mno kwani wapiga kura waliosajiliwa ni 59,000.Uchaguzi uliahirishwa katika eneobunge hili kufualia kifo cha Mgombea wa chama cha Jubilee(Leonard Mwamba) majuma mawili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 8/8/2017.

Iliandikwa na Okello Kevin

Leave a Reply