WAWANIAJI VITI MBALIMBALI MACHAKOS KUPIGWA MSASA

Viongozi wa makanisa, mashirika ya kijamii na washika dau wengine kutoka  kaunti ya Machakos wamekutana kujadili maswala yanayoathiri mwananchi na kuafikia kuwahamasisha wananchi kuhusu kile kinachotarajiwa kwa viongozi wao.
Wakiongozwa na Dakt. Edward Nzinga chini ya mpango wa Mulika Initiative wameafikia kuwajulisha wagombea viti mbalimbali vya uchaguzi matarajio yao kwa wananchi.
Sasa wanalenga kuandaa vikao vya kuwapiga msasa wale wanaowania viti mbalimbali ili kubaini viongozi wenye maadili.
Mpango wa kuwahoji viongozi ni bora mno kulingana na mwenyekiti wa NCCK tawi la Machakos Edward Nzinga viongozi hawa wanafaa kushiriki katika zoezi hili wakihoji mkenya amechoka kudanganywa na kiongozi mbinafsi.
Na iwapo kuna wale watakaokosa kushiriki basi sio viongozi wema
Tangu kuanzishwa zoezi la kuwapiga msasa wawaniaji viti mbalimbali wamebaini kuwa baadhi ya viongozi wanatoa ahadi ambazo wanashindwa kutekeleza baada ya kuchaguliwa hivyo wamebaini mbinu ya kukabiliana na hili, kuandaa tena vikao vya mara kwa mara na watakaochaguliwa ili kuwashurutisha kutekeleza ahadi hizi.
Sheikh Ahmed Ramadhan Musa naibu Imamu wa Machakos naye anawataka wakenya kuishi kwa upendo wakati tunapoelekea kwa uchaguzi.