MIGOGORO ZA MASHAMBA BUSIA

MAWAKILI WAHIMIZWA KUWASHAURI WATEJA WAO KATIKA MIGOGORO YA MASHAMBA VILIVYO ILI KUEPUKA MAKESI MAHAKAMANI

HI NI KWA MUJIBU WA JAJI WA MAHAKAMA YA BUSIA, KITENGO CHA MAZINGIRA NA ARDHI PATRICK OKENGO AMBAYE ALISEMA HAYA WAKATI WA HAFLA YA UHAMASISHO WA HUDUMA ZA MAHAKAMA KWA UMMA

USEMI HUO ULIUNGWA MKONO NA NAIBU KAMISHNA WA GATUZI NDOGO LA MATAYOS KIPCHUMBA RUTTO AMBAYE ALIWARAI WANANCHI KUZINGATIA NJIA M’BADALA ZA KUSULUHISHA MIZOZO ZA MASHAMBA BILA KYELEKEA MAHAKAMANI

WAKATI HUO HUO, MSAJILI ARDHI KAUNTI YA BUSIA WILFRED NYABERI AMEWAHATADHARISHA WAKAAZI WA BUSIA DHIDI YA KULAGHAIWA NA MATAPELI WA MASHAMBA NA KUWATAKA KUZURU AFISI YAKE NA ZA CHIFU KATIKA SHUGHULI ZOZOTE ZA MASHAMBA