Kila kulipokucha miezi michache iliyotupa kisongo, wazazi waliokuwa na wana shule za upili walikuwa wanajawa na wa wasi wasi. Ungelimpata mzazi kwa barabara ungelipigwa na butaa, huku ukijiuliza ama alizozionyesha ni dalili za kupangawa ama ni maji yaliyozidi unga.
Kilichokuwa kikiwasumbua sio kingine wala kisa, ambacho wahenga walisema baada ya kisa mkasa na panapo moshi basi kuna moto. Kilichowatawala ni hofu, wakiomba na kutumai wanao hawatahusika kamwe kwenye visanga vilivyokuwa vikizibusu shule kila kuchapo.
Na ni kweli Mungu haengemei upande mmoja na wanja wake anawadhamini. Visa vilipungua huku Waziri Mkuu wa Elimu Dakitari Fred Matiang’i akisukumwa kuzifunga zile shule zilizobakia.
Hata hivo, kwa baadhi yazo wanafunzi walikuwa wameyatekeleza tayari maafa na maji wakayamwaga, na muda wa kuyazoa haukuwa. Hivi sasa duru ya mgambo imelia, na wazazi wanatarajiwa kuandamana na wanao kule shuleni ambako kesi zawangoja.
Kuna wale ambao mkono mrefu wa serikali uliwafikia kisha wakatiwa mbaroni. Kesi zao zingafukuliwa huku wengine wakiachiliwa kwa dhamana. Hata hivyo baadhi yao wameruhusiwa kurudi shuleni huku kesi zao zikitarajiwa kushughulikiwa mwishoni mwa mwaka.
Kuna wale wazazi ambao wanao kamwe hakushiriki kuyatekeleza yale lakini mtego wa panya unasao waliomo na wasiokuwemo haukuwaacha nyuma. Badala yake, umevurutia chini kama kitambaa kilichokwama kwenye guriudumu la gari.
Kwa sasa, watalazimika kulipa karo mingi, kiwango fulani cha pesa kusimamia gharama kubwa kutokana na uharibifu walioufanya, mzingo mzito waliotwika na wanao. Na haya yanapotokea tunalo swali moja tunapaswa kujiuliza, ni nani wa kulaumiwa?Ni walimu, wazazi, serikali, wananchi ama sisi sote?
Jinsi sisi huzichunga simu zetu za kutomasa ndivyo tunastahili kuzifanyia shule. Mwanafunzi aliyeshiriki kupanga yale hadi shule ikateketezwa kuna uwenzekano hakuonekana? Na ikiwa alionekana mwenye aliyasikia yale hakulipiga debe?
Haya sio maswali tunayoweza kuyajibu kwa kupitishiana lawama. Badala yake, wazazi, wakuu wa elimu, viongozi wa wanafunzi na walimu wanastahili kulikalia hili chini na kulichimbwa kwa undani wakiwinda suluhu. Haya nafahamu si rahisi kuafikia kwa kuwa sheria sio kama chakula ambacho upikwa kwa moto. Lakini kunao waliobarikiwa na uongozi, wenye Uwezo wa kulitazama
Wasemapo wahenga usipoziba ukuta utajenga ukuta ni kweli. Watoto wetu, dada na kaka wametuingiza kwenye shimo la tewa, letu ni kulia tusipanguzwe machozi tu mbali hili shimo lizibwe.
Ombi langu kwa wazazi ni wazungumze na wanao na kuwapa mawaidha huku wakiwadokezea umuhimu wa elimu na adhari za kushiriki kwenye visanga hivyo. Kwa upande wa pili wanafunzi wazame kwenye vitabu na kuyatupilia mbali ya kale.