Binadamu mbona awe mnyama?

Kuna kisa fulani, ukipenda kisanga ambacho jana kiliwaacha wengi kinywa wazi baada mtoto mchanga wa umri wa majuma mawili kupatikana ametupwa ndani ya shimo la choo.

Wakaazi wa Bobong katika eneo la Narok  walidai kuwa, walisikia kilio cha mtoto na baada ya kusikiza kwa makini waligundua sauti ile ilikuwa inatoka mle ndani.

Jambo hilo liliwatia wengi wasiwasi na kuanza kutafuta namna ya kukiokoa kiumbe kile kisichokuwa na hatia yoyote.

Waliozungumza na wanahabari walidai kuwa kuna mwanamke wa umri wa makamo aliyengia mle chooni huku amebeba mtoto. Baada ya kutoka hakuwa naye, na alionekanan kwa barabara ametimua mbio kama aliyekuwa anaogopea kitu. Hapo walianza kuchimba kando wakitafuta namana ya kumwokoa.

Wananchi walipong’amua muda haukuwa unawaegemea walitafuta mbinu ya pili, kukiteremsha chuma walichokitumia kama kamba na walipobahatika kumtoa nje, msamaria mmoja alijitokeza na kuleta gari lake wamkibishe hosipitalini.

Itabainika wazi kuwa hiki sio kisa cha kwanza kutokea. Kuna visa kadha wa kadha ambapo watoto wameripotiwa kutupwa mapipani, vyooni ama pia kuachwa kwenye vyumba vya kukodisha.

Lakini swali ni je, mbona mama amzae na kumtupa mtoto asiye na hatia? Ikiwa hakuwa amejipanga kulea mbona akaipata ile mimba na kunazo njia tofauti za kupanga uzazi? Na kama ilikuwa ni ‘anjali’ na hamtaki, mbona asiombe usaidizi?

Kuna wale wanawake ambao, kwa namna moja hama nyingine hawewezi kupata watoto. Hili ni kutokana na shinda kwenye mfuko wa uzazi (uterus) ama, kabisa hana uwezo wa kupata mimba, yeye ni tasa na. Hawa huwa wanaomba mwenyezi Mungu angalau awabariki na mtoto mmoja. La kushangaza ni kuwa, wakati wanaomba wapate watoto wengine wanawatupa.

Siwezi nikasema kizazi cha sasa hakielewi maana ya ulezi, na kidogo nitauasi msemo wa wahenga kuwa ‘uchungu wa mwana haujuao ni mzazi’. Ikiwa methali hii ina uzito wake, basi hao wanaotupa watoto wanaweza kuwa sio wazazi? Na kama sio wazazi tutawaweka kwenye kundi lipi? Ama kweli, kuzaa wameweza lakini kazi  imewashinda?

Watakwambia wanaodhamini kuzaa kuwa miezi tisa ni kama miaka na mikaka na uchungu wa kupoteza mwana unaumiza roho kuliko kupoteza kazi. Wazo ambalo nakumbaliana nalo. Kumbuka Maulana anatazama hivyo usimwonyeshe kitambi, huenda akawaza na kuwazua na pipango yake haina makosa.

Ingekuwa vyema wanadada kudhamini watoto, hiyo ni baraka na haitupwi kwa kuwa baraka itokapo laana uingia. Watoto sio nguo, hawapatikani sokoni ama dukani, linda wako kama dhahabu na Maulana atakunyeshea baraka. Kumbuka, panapo nia pana njia.

Haya sia mawazo ya KUTV, ni mawazo yangu binafsi. gmmunyoki@gmail.com