Kijana mmoja wa umri wa makamo ijumaa iliyopita alijipata mashakani baada ya kuvumaniwa na mwenye boma mchana akikata jasho baada ya kusherehekea asali ya kuiba.
Kulingana na wakaanzi wa mtaa wa Kiwanja bibi huyo ambaye jina lake limebanwa alimkaribisha kijana huyo mwendo wa masaa ya saa nane mbila kujua bwanake hakuwa ameenda mbali.
Wawili hao walipatikana wangali wanajivinjari jambo ambalo lilizoa ungomvi kati ya fahali hao wawili. Na kama kawaida, umati ulianza kukusanyika baada ya kuvutiwa na kukaribia kuitazama sinema ile.
Jambo hilo liliwaudhi wenyeji waliodai tamaa ya pesa ilikuwa imemwingia mwanamke huyo na kulifanyanya ‘dhehebu lake’ simu ya kutomasa huku akibandikwa jina ‘mjinga’ kwa kunajisi ndoa yake.
Kulingana na wakaanzi, vituko vilianza pale mwanaume huyo kisadifa alirudi nyumbani mapema kuliko kawaida yake, mwendo saa kumi na moja.
Alipoingia ndani aliwapata wawili hao, dume mla cha wenzio na bibi wake wikipeana kwaheri huku mwanaume huyo akiyavalia mavazi yake, na hapo vita vikazuka.
Hata hivyo, umati uliokusanyika ulishindwa kuzima vita hivyo na cheche za matusi hadi pale maghulamu kadha walipoamua kuingilia kati na kuwashikwa kuzuia maafa yaliyokuwa yananukia.