Waititu apendekeza siku ya chaguzi za vyama iwe siku ya mapumumziko

Akizungumza hii leo kwenye maonjiano na redo moja hapa nchini Kenya, Ferdinad Waititu, Mbunge wa Kabete amesema kuwa ataupeleka mswada mbungeni akiomba siku ya changuzi za vyama iwe siku ya mapumziko hapa nchini.

Waititu alisema kuwa, uchanguzi wa cha chama utaonekana kuwa wa haki ma uwazi iwapo tume ya Uchanguzi na Mipaka (IEBC) itahusishwa kikamilifu.

Kulingana na Waititu, Tume hiyo inahistahili kuendesha uchanguzi wa vyama jinsi uchanguzi mkuu unavyofanyika na kisha mshundi atakeygombea nafasi ya kiti kile kupitia tiketi ya chama kutangazwa.

Hata hivyo, mbunge huyo alikiri kuwa kunao wasiwasi mwingi kwenye chama cha kipya cha Jubilee akisema kuwa, watu wanaogopa wasije wakakosa tikiti na kulazimishwa kutogombea wadhifa wanaoutamani baada ya sheria inayowasuta wanachama kukigura chama baada ya kukosa tikiti kupitisha.

Akiondezea zaidi, Waititu alisema Jubilee wako na furaha baada ya vyama tanzu vilivyowapeleka wabunge na viondozi kadha wa kadha bungeni kuungana na kutengeneza chama kimoja watakachukitumia kwenye uchanguzi wa mwaka wa elfu mbili na kumi na saba.