Tume ya uchaguzi IEBC inasema itaweka wazi kabla ya mwishoni mwa mwezi huuu mikakati iliyowekwa kuhakikisha uchaguzi ujao unaandaliwa kwa njia huru.
Katika taarifa, tume hiyo imesema inaangazia sheria mpya kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyofanyiwa marekebisho hivi maajuzi.
Kwenye waraka huo, mkurugenzi wa mawasiliano Ander Limo anasema kunahitajika mabadiliko kadhaa ili kuhakikisha uchaguzi huo utaandaliwa Agosti mwaka ujao.