NILIMSAIDIA MBOSSO SASA AMEKUWA STAA ANANIBLUE TICK, ATETA D DAMMY AKIWA KENYA

By Labaan Shabaan

 

D Dammy Serious msanii kutoka Tanzania ambaye yuko kwenye media tour Kenya ya nyimbo yake ‘nimeboycott’ ameteta kuhusu nyota wa wcb Mbosso kumpa blue ticks licha hata yeye kuwa mshikaji wake wa karibu kipindi cha awali wakiwa wanakula mbirimbi na kumeza mate wengine wakila nyama. 

D dammy Serious ambaye ni mnenguaji mauno na produsa hana raha na haelewi kwa nini Mbosso amekataa kupokea simu zake ama kujibu jumbe alizomtumia kuhusu kufanya video ya nyimbo walioimba kwa jina ‘ibaki love story.’ 

Akizungumza na KUTV nchini kenya Dammy amesema wametoka mbali na mbosso. Pia wamefanya kazi pamoja na kuwa amemfanyisha collabo nyingi kabla mbosso hajatamba.

‘’hata kama hanizungumzii kwenye media najua nafsi yake inamsuta kwamba mpaka kufika hapa kuna mtu anaitwa D Dammy serious…’’ 

Dammy ameandaa miziki ya J.I Wa Kidato Kimoja, Ruby, Pasha, Madam Flora, Maringo Mzee Wa Ndolela, Steve Rnb, Rose Muhando, Nandy, Masanja Mkandamizaji  kutaja tu baadhi. 

Tazama mahojiano ya D Dammy hapa…