Seneti hii leo imemwamuru Waziri wa Afya Cleopa Mailu ahakikishe kuwa viongozi wa muungano wa madaktari (KMPDU) ambao walifungwa jela jana wameachiliwa .
Kwa upande mwingine, Seneti pia imemtaka Mailu ashauriane na Mkuu wa Sheria kuhusu njia bora ya kusitisha mgomo wa madaktari haraka iwezekanavyo na kisha arudi na majibu mbele ya seneti hapo kesho.
Wakati huo huo madaktari katika hospitali za kibinafsi wametisha kujiunga na wenzao katika mgomo kesho jumatano, na hivyo kusitisha shughuli zote za matibabu.
Hiyo jana baada ya viongozi hao kuukumiwa jela kifungo cha mwenzi mmoja, madaktari waliandaa mkutano kwenye klabu moja huko Railways kama ishara ya umoja na viongozi wao.
Madakitari hao walitishi kutumia siku hizo 30 kuandamana ama kufanya mikutano mara kwa mara kuonyesha umoja wao.
Hata hivyo mkutano wao uliimuliwa na maafisa wa polisi waliofika pale.
Mazungumzo yatarajiwa kuendelea
Mazungumzo kati ya madaktari na waajiri wao yataendelea, licha ya mgomo ambao umedumu kwa muda wa mwezi mmoja, na kutiwa mbaroni kwa viongozi wa muungano wa madaktari.
Kulingana na tume ya kutetea Haki za Binadamu na muungano wa COTU ambao ndio wapatanishi, viongozi hao saba hawange epuka kifungo hicho cha mwezi mmoja ndani ya jela, licha ya kujitahidi kushawishi serikali