Shughuli za kujiandikisha kama wapiga kura zinatazamiwa kufika tamati hii leo kulingana na muda uliowekwa na Tume Huru ya Haki na Uchanguzi na Mipaka (IEBC)
Leo ikiwa siku ya mwisho ya usajili wa wapiga kura, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imesema kuwa imepata kampuni moja ambayo itakagua sajili ya wapiga kura kwa siku 30.
Rasi Masudi ambaye ni mkurugenzi wa Alimu ya Umma amasema kuwa ukaguzi huo umechelewa kutokana na mtafaruku wa vifungu vya sheria.
Shughuli za kusajili wapiga kura hata hivyo zilijawa na maswali baada ya watu kutoka NYS kupatikana wakisajili watu hio jana na kuibua maswali tata.
Uamuzi wa mahakama utaadhiri pakubwa uchanguzi mkuu
Tume ya Uchaguzi na Mipaka imesema kuwa uamuzi wa mahakama wa kufutilia mbali kandarasi ya kununua vifaa vya uchaguzi, itaathiri pakubwa uchaguzi mkuu ujao.
Afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa uamuzi wa Jaji George Odunga unamaanisha kuwa shuguli zote ambazo tume hiyo imefanya katika miezi 3 iliyopita yatatupiliwa mbali.
Aidha Chiloba amesema kuwa uamuzi kuhusu ununuzi wa makaratasi ya kura, sanduku za kura, ukaguzi wa hesabu, usajili wa wapiga kura utaathiriwa.