Mbunge wa Ugunja, Opiyo Wandayi, amedai kuwa wakuu wa tume ya uchanguzi, Tume Huru ya Haki na Mipaka, (IEBC) wanaostaafu hawastahili kamwe kupewa ata shilingi moja kama ilivyopendekezwa na kamati teule baada ya wakuu hao kung’atuka mamlakani kufuatia shinikizo zilizowaandama.
Opiyo aliyasema haya jumapili iliyopita, tarehe 4 mwezi wa tisa, huku akiongezea kuwa hakuna kipengee ata kimoja kwenye katiba ya Kenya kinachowaruhusu watu kulipwa mshahara kutokana na kazi ambayo hawajaifanya.
Opiyo aliongezea kuwa, kumbaliano baina ya makamishina na kamitii hayakuwa ya halali na kwa hivyo hawastahili kulipwa.
Mbunge huyo alimwomba Mwendeshaji Mkuu wa kesi za Serikali, Githu Muigai, alizingatie ombi lile akidai kuwa kuwalipa sio haki.
Shinikizo la wakuu wa Tume ya Uchanguzi lilikuwa limeongozwa na upinzani baada ya tume hiyo kutajwa kama isiyokuwa imejipanga kikamilifu kusimamia uchanguzi ujao wa mwaka wa 2017 na changuzi zingine.
Kukosekana na imani kwa wakuu hao kulipelekea maandamano kwenye ofisi za tume ya uchanguzi kama njia moja ya kuwango’a ofisini. Kutokana na adhari zake, kamati iliundwa kushughulikia swala hilo na mwishowe ripoti ikawasilishwa mbungeni.
Kwa sasa, wahusika wako mbioni kubaini ni hakina nani watakaochukua hatamu baada ya makamishina hao kungo’oka mamlakani kabla ya mwisho wa mwezi wa tisa.